kimataifa

KOCHA CHELSEA AFIKIRIA KUONGEZA BEKI WA KATI

admin February 6, 2021 6:47 am

 INAAMINIKA kwamba nyota wa kikosi cha RB Leipzig,  Dayot Upamecano ni miongoni mwa orodha ya majina yaliyopo kwenye mpango wa Kocha Mkuu wa Chelsea,  Thomas Tuchel. 

Ripoti zinaeleza kuwa Tuchel ambaye ni mrithi wa mikoba ya Frank Lampard macho yake kwa upande wa usajili yanatazama nyota ambao wanashiriki Bundesliga na anahitaji beki wa kati.


Tuchel tayari ameanza kazi ndani ya Stamford Bridge huku akionekana kuleta mabadiliko ndani ya timu na ana matumaini ya kuboresha zaidi kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao..


Kwa mujibu wa Bild,gazeti la Habari la Ujerumani limeripoti kuwa Tuchel katika akili yake kuna majina ya mabeki watatu ambao ni Niklas Sule na David Alaba wa Bayern Munich pamoja na Upamecano.


Alaba mwenye miaka 28 pia anatajwa kuwaniwa na Liverpool pamoja na Liverpool ambao nao wanawania saini yake.

MTAMBO WA MABAO YANGA WATOA KAULI YA MATUMAINI KISA FISTON KAZE AIPA NAFASI SIMBA KUTUSUA KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply