Yanga SC

NYOTA YANGA PRINCESS AFIKIRIA MABAO 100

admin February 10, 2021 3:47 am


 ASHA  Masaka, ‘Ashamabao’ mshambuliaji wa timu ya Yanga Princess amesema kuwa kwenye kila mashindano huwa anafikiria kufunga mabao 100.

Kwa sasa Kwenye Ligi ya Wanawake Tanzania,  Asha ni namba mbili kwa utupiaji ambapo Oppa Clement wa Simba Queens na Fatma Mustapha wa JKT Queens namba moja wakiwa wametupia mabao 20.

Yeye Asha ikiwa ni msimu wake wa kwanza ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Edna Lema ametupia mabao 15.

Kikosi cha Yanga Princess kinaongoza Ligi Kuu ya Wanawake baada ya kucheza mechi 11 na kibindoni kina pointi 31.

Asha amesema:”Huwa nafikiria kufunga mabao kuanzia 100 jambo ambalo linanifanya nazidi kupambana ndani ya Uwanja,”.

INGIZO JIPYA YANGA HATIHATI KUIVAA MBEYA CITY MEDDIE KAGERE:USHINDANI BONGO NI MKUBWA KILA IDARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply