Yanga SC

YANGA KUIBUKIA MBEYA LEO, YAWAOMBA MASHABIKI WAJITOKEZE KUWAPOKEA

admin February 11, 2021 4:47 am

 

KIKOSI cha Yanga leo kinatarajia kuanza safari kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City. 

Mchezo huo wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ambapo Yanga wamewaomba mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kuwapokea leo mchana Uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya.

Walipokutana Uwanja wa Mkapa, Yanga ilisepa na pointi tatu muhimu kwenye mzunguko wa kwanza baada ya kushinda bao 1-0 lililopachikwa na Lamine Moro. 

Februari 13 watakutana uwanjani wakiwa na mtambo wao wa mabao Fiston Abdulazack ambaye ni ingizo jipya ndani ya vinara hao wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 44.

Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kupata matokeo chanya.

NYOTA WANNE WA AZAM FC KUWAKOSA COASTAL UNION LEO KAMA UNAMPENZI HII INAKUHUSU ..PATA ZAWADI YA VALENTINE NA UUMPENDAYE …SIMPLE TU NA Infinix…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply