Namungo FC

WALIOKWAMA ANGOLA KUREJEA LEO, MMOJA ABAKI

admin March 2, 2021 6:47 am


 LEO Machi 2, wachezaji wa kikosi cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco wanatarajiwa kuwasili ardhi ya Bongo wakitokea nchini Angola.

Wachezaji hao wawili ni Lukas Kikoti na Hamis Fakhi ambao walianza safari jana kwa kupitia Ethiopia wakitokea Angola walikokuwa wameshikiriwa karantini kwa zaidi ya siku 16.

Walikwama wakati walipkwenda kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya 1 de Agosto pamoja na mwingine Fred Tangalo ambaye amebaki Angola.

Tangalo ambaye ni ingizo jipya kutoka ndani ya kikosi cha Lipuli amebaki Angola kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa majibu yake ya Corona bado hayajatoka.

 Namungo imetinga hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho na ipo kundi D.


LIVERPOOL YAHITAJI SAINI YA KIUNGO WA UDINESSE VIDEO: AISHI MANULA ALIVYOKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUPATA MAJERAHA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply