Namungo FC

SHAMTE AREJEA KUWAVAA WAMOROCCO

admin March 9, 2021 12:47 pm

 

KUELEKEA mchezo wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika, dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa kesho Jumatano, kikosi cha Namungo kimezidi kuimarika baada ya beki wa kulia wa kikosi hicho, Haruna Shamte kurejea akitoka kwenye majeraha.

Shamte alipata majeraha hayo katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Mbeya City uliopigwa Jumapili ya Februari 28, mwaka huu na kupelekea kukosa michezo ya Ligi Kuu iliyofuata dhidi ya Mwadui na Kagera Sugar.

Akizungumzia maendeleo ya beki huyo, Ofisa habari wa Namungo, Kindamba Namlia amesema: “Kuelekea kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Raja Casablanca, wachezaji wote wako tayari na habari njema ni kurejea kwa beki wetu wa kulia, Haruna Shamte ambaye ametoka kwenye majeraha na tayari ameanza mazoezi pamoja na wenzake,”


KAZE AWAACHIA YANGA UJUMBE HUU NI RASMI, MWAMBUSI TENA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply