Taifa Stars

NYOTA WAWILI TAIFA STARS WAUMIA, NCHIMBI NA BRYSON

admin March 12, 2021 7:47 am


 KIKOSI cha Taifa Stars kikiwa kinaendelea na maandalizi ya mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya na za kufuzu AFCON dhidi ya Libya na Equatorial Guinea, nyota Ditram Nchimbi anatibu majeraha.

Mshambuliaji huyo pamoja na David Bryson wote wawili wanatibu nyama za paja.

 

Daktari wa Taifa Stars, Richard Yombo, amesema: “Wachezaji wawili wamepata majeraha ya nyama za paja ambao ni Ditram Nchimbi na David Bryson,”.

 

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen, amesema: “Tunashukuru Shirikisho kwa kutuwekea mechi mbili za maandalizi dhidi ya Kenya kabla ya kuvaana na Equatorial Guinea


“Kikubwa tumefanyia kazi kuanzia eneo la ulinzi, kiungo na ushambuliaji ili kupata matokeo mazuri katika michezo ya kufuzu.”

 

Taifa Stars ikiwa Kundi J, inashika nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi nne. Vinara ni Tunisia wenye kumi, huku Equatorial Guinea wakiwa na sita, wakati Libya wakishika nafasi ya mwisho kwa kuwa na pointi tatu.

KISINDA AWA MUHIMILI WA YANGA KWA MIPANGO NDANI YA UWANJA ISHU YA NTIBANZOKIZA KUSAINI KCCA UKWELI HUU HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply