Yanga SC

KISINDA AWA MUHIMILI WA YANGA KWA MIPANGO NDANI YA UWANJA

admin March 12, 2021 6:47 am


TUISILA Kisinda nyota wa kikosi cha Yanga ameonekana kuwa ni mhimili wa kikosi hicho ndani ya uwanja ambacho kinaongoza ligi baada ya kucheza jumla ya mechi 23 na kukusanya jumla ya pointi 50.


Kisinda ameonekana kuwa ni mhimili wa kikosi hicho katika kusaka ushindi kwa kuwa kwenye jumla ya mabao 36 ambayo yamefungwa na timu hiyo amehusika kwenye mabao 10.

Ingizo hilo jipya kutoka Klabu ya AS Vita ya Congo limetupia jumla ya mabao manne, pasi nne za mabao na kusababisha penalti mbili ambazo zilileta mabao.

Pia Kisinda ambaye anasifika kwa kuwa na spidi ndani ya uwanja amekuwa akicheza kwa maelewano makubwa na wachezaji wenzake ndani ya uwanja ikiwa ni pamoja na Fiston Abdulazack ambaye ni ingizo jipya, mshikaji wake Tonombe Mukoko  pamoja na Carlos Carlinhos ambao hawa wote amewapa pasi mojamoja ya bao.

Jukumu la kupiga penalti ambalo amekuwa akipewa ndani ya uwanja lilikuwa gumu kwake Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ambapo penalti yake aliyopiga iliishia kwenye mikono ya kipa wa Coastal Union , Abubakari Abasi.


KATWILA AKWAMA MBELE YA AZAM FC NYOTA WAWILI TAIFA STARS WAUMIA, NCHIMBI NA BRYSON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply