Kawempe Muslim Ladies CECAFA
Habari za michezo

Kawempe Muslim Ladies Mabingwa CECAFA: Watavunja Mwiko Ligi ya Mabingwa Afrika?

Vardo September 1, 2026 6:01 pm

Kawempe Muslim Ladies Mabingwa CECAFA: Watavunja Mwiko wa Afrika Au Watakwama Kama Wengine?

Kawempe Muslim Ladies imeweka historia mpya baada ya kutwaa ubingwa wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya Police Bullets katika fainali iliyopigwa jijini Kigali, Rwanda. Bao la ushindi la Agnes Nabukenya katika dakika ya 100 limeifanya timu hiyo kuwa mwakilishi wa kwanza kutoka Uganda kukata tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake.

Hii ni mara ya pili kwa Kawempe kushiriki michuano ya CECAFA (baada ya kushika nafasi ya tatu mwaka 2024), na safari yao ya mwaka huu imekuwa ya mfano.


Njia ya MOTO: Mwenendo wa Kawempe Jijini Kigali

Kawempe haikupata tiketi hii kwa bahati mbaya, bali kwa uwezo mkubwa na nidhamu ya mchezo. Katika mechi zake nne za kampeni hiyo:

  • Mechi za Kundi B: Ilianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Commercial Bank of Ethiopia (CBE), kisha ikaiadhibu FC Ujeco ya Djibouti mabao 8-0 na kuongoza kundi.

  • Nusu Fainali: Ilishinda 3-0 dhidi ya CBE.

  • Fainali: Ilichapa Kenya Police Bullets 1-0.

Jumla ya mabao 13 yalifungwa bila kuruhusu bao hata moja katika lango lao—takwimu zinazoontsha ubora wa safu yao ya ulinzi na ushambuliaji.


Mtihani Mzito Fainali za Afrika

Swali kubwa analojiuliza kila mdau wa soka la wanawake Afrika Mashariki ni: Je, Kawempe itaweza kudumisha kiwango hiki inapokutana na miamba ya Afrika?

Tangu kuanzishwa kwa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake mwaka 2021, timu nyingi za CECAFA zimekuwa zikionyesha utawala mkubwa kimkoa lakini zikigonga mwamba hatua ya makundi barani Afrika. Timu kama Vihiga Queens (Kenya, 2021), JKT Queens (Tanzania, 2023 & 2025), na CBE (Ethiopia, 2024) zote ziliishia hatua ya makundi.


Funzo Kutoka Kwa Simba Queens (2022)

Simba Queens ya Tanzania ndiyo timu pekee kutoka ukanda wa CECAFA iliyowahi kuweka rekodi ya kipekee Afrika. Mwaka 2022 nchini Morocco, baada ya kutawala CECAFA kwa kufunga mabao 18 na kuruhusu moja pekee:

  1. Walipoteza 1-0 dhidi ya wenyeji AS FAR katika mchezo wa kwanza.

  2. Walipambana na kuzifunga Determine Girls (Liberia) 2-0 na Green Buffaloes (Zambia) 2-0 na kutinga Nusu Fainali.

  3. Walitolewa na mabingwa Mamelodi Sundowns (1-0) na kuishia nafasi ya nne barani Afrika.

Simba Queens ilionyesha kuwa ili ufanikiwe Afrika, unahitaji ustahimilivu, uimara wa mbinu, na uwezo wa kukabiliana na presha kubwa kutoka klabu za Kanda ya WAFU, UNAF, na COSAFA.


Kocha Ayub Khalifa Na Maandalizi Ya Vita Mpya

Akizungumza baada ya kutwaa ubingwa, Kocha Mkuu wa Kawempe Muslim, Ayub Khalifa Kiyingi, alisifu juhudi za wachezaji wake:

“Tulicheza na timu ngumu lakini niwapongeze wachezaji wangu wamefanya kazi kubwa kwa juhudi na kujitoa sana.”

Ili Kawempe ifanye vizuri zaidi ya waliotangulia, italazimika kuhifadhi msingi wa kikosi chake kilichotwaa ubingwa Kigali, huku ikiongeza uzoefu, kasi ya maamuzi, na uwezo wa kustahimili michezo yenye ushindani wa juu zaidi.

Ukaribu wa Wifi na Shemeji: Fatma Mkambala Aweka Wazi Uhusiano Wake na Mke wa Jux, Priscilla Ojo Siri Yafichuka! Sababu ya Mzize na Job Safarini Botswana Huku Hawachezi Dhidi ya Gaborone Utd