Simba SC

WAARABU WA MISRI WAIPIGIA HESABU SAINI YA LUIS

admin March 26, 2021 4:47 am

 


KLABU mbili za Afrika kutoka Misri zimeingia anga za kuwania saini ya nyota wa Simba, Luis Miquissone ili kupata saini yake.

Waarabu hao wa Misri ni Pyramids na Al Ahly ambazo zinataja kufuatilia kwa karibu mwendo wa nyota huyo mwenye mabao mawili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha wa Al Ahly, Pitso Mosimane aliwahi kufanya kazi na Luis na aliweka wazi kwamba miongoni mwa wachezaji ambao walimpa tabu alipokutana nao Uwanja wa Mkapa alikuwa ni Luis.

“Luis ni mchezaji mzuri na anajua namna ya kufanya akiwa uwanjani hasa pale anapotafuta matokeo kwa ajili ya timu.

“Ninamtambua kwa sababu nimefanya naye kazi na anajua kukaa kwenye nafasi,” .

Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe amesema kuwa taarifa hizo bado hazijafika mezani.

EQUATORIAL YAIFUNGASHIA VIRAGO STARS AFCON COUTINHO, GRIEZMANN, UMTITI WAWEKWA KWENYE HESABU ZA KUUZWA BARCA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply