epl

MANCHESTER UNITED WATAJA SABABU ZA KUTINGA NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE

admin April 16, 2021 7:47 am

 

OLE Gunnar Solskjaer,  Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa sababu kubwa aliyewapa ushindi mbele ya Granada ni nidhamu ya wachezaji pamoja na uwezo wa kutumia nafasi ambazo walizipata.

United ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Granada katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya pili na kupenya mpaka nusu fainali kwa jumla ya mabao 4-0.

Ni Edinson Cavan dakika ya 6 na Jesus Vallejo dakika ya 90 alijifunga na kuwafanya United kukata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Europa League wakiwa Uwanja wa Old Trafford. 

Wanakwenda kukutana na Roma katika hatua ya nusu fainali ambayo ilishinda mbele ya Ajax kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya robo fainali ya jana ubao wa  Stadio Olimpico kusoma Roma 1-1 Ajax.

Ni Brian Brobbey dakika ya 49 alianza kufunga kwa Ajax na liliwekwa usawa na Edin Dzeko dakika ya 72 na  kufanya ngoma iwe 1-1.

MANULA AINGIA KWENYE VITA NA MAKIPA WATANO AFRIKA VIDEO: MTIBWA SUGAR SIMBA NI TIMU KUBWA AFRIKA, YAYEYUSHA NDOTO ZA UBINGWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply