kimataifa

ALABA AKUBALI KUTUA REAL MADRID

admin April 23, 2021 2:48 pm

 


BEKI wa Bayern Munich, David Alaba amefikia makubaliano ya kujiunga na miamba ya soka barani ulaya, Real Madrid ifikapo wakati wa majira ya kiangazi msimu huu.

 

Beki huyo kitasa atasaini mkataba wa miaka mitano na Los Blancos ambao utamuweka nchini Hispania hadi majira ya joto ya mwaka 2026.

 

Taarifa hii inamalizia sakata la muda mrefu juu ya hatma ya nyota huyo ambaye mapema mwaka huu alithibitisha kuwa angeondoka nchini Ujerumani lakini haikufahamika angejiunga na klabu ipi.

 

Nyota huyo wa kimataifa Australia ambaye ameitumikia The Bavarians kwa takribani miaka 13 kwa mafanikio, alikuwa akihusishwa kwa muda mrefu sasa na kuhamia nchini Hispania huku Barcelona nayo ilikuwa ikiwania saini yake.

NAMUNGO YAAHIDI KUPAMBANA MCHEZO WAO WA MWISHO SIMBA: KILA MMOJA ASHINDE MECHI ZAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply