Simba SC

SIMBA: KILA MMOJA ASHINDE MECHI ZAKE

admin April 23, 2021 3:47 pm

 MOHAMED Hussein, ‘Zimbwe’ nahodha msaidizi wa kikosi cha Simba amesema kuwa kwa sasa kila mmoja ashinde mechi zake ili kuweza kupiga hesabu mwisho nani atachukua taji la Ligi Kuu Bara.

Kumekuwa na ushindani mkubwa msimu huu kwenye mbio za ubingwa ambapo vita ya Simba ambao ni mabingwa watetezi dhidi ya watani zao wa jadi Yanga imezidi kuwa kubwa kutokana na tofauti ya pointi mbili ambazo wanazo kwa sasa.

Yanga ni kinara akiwa amecheza jumla ya mechi 26 kibindoni ana pointi 57 huku Simba ikiwa nafasi ya pili na ina pointi 55 ila imecheza mechi 23 na ina mechi tatu kuweza kuwa sawa na watani hao ambapo watakutana Uwanja wa Mkapa, Mei 8.

Akizungumza na Soka la bongo, Zimbwe amesema kuwa wao kwa sasa hesabu zao ni kwenye mechi zao hawatazami timu nyingine inafanya nini, lazima kila mmoja ashinde mechi zake.

“Sisi hatuangalii mwenzetu kafanya nini kwenye mechi zake ama aina gani ya matokeo ambayo yanapatikana ambacho tunakitaka ni kuona kwamba kila mmoja anashinda mechi zake, hakuna jambo lingine.

“Ushindani ni mkubwa kwenye ligi hilo lipo wazi nasi pia tunapambana kuona katika mechi zetu tunapata pointi tatu, mashabiki wazidi kutupa sapoti,” amesema.

ALABA AKUBALI KUTUA REAL MADRID FEI TOTO AREJESHA MATUMAINI YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply