Pacome Zouzoua Yanga SC
Yanga SC

Hali ya Pacome Zouzoua Yanga SC: Ali Kamwe Afunguka Maendeleo Yake Kiafya

Vardo August 30, 2026 3:59 pm

Klabu ya Yanga SC imetoa taarifa mpya kuhusu maendeleo ya afya ya kiungo mshambuliaji wake hatari, Pacome Zouzoua, ambaye bado yupo kwenye kipindi cha kujiuguza majeraha ya mguu.

Msemaji wa Yanga SC, Ali Kamwe, amethibitisha kuwa hali ya Pacome inaendelea kuimarika kwa kiwango kizuri, ingawa bado anatumia magongo kumpa msaada wakati wa kutembea. Kamwe alieleza kuwa nyota huyo hajasepa nchini na anaendelea kupatiwa matibabu ya karibu chini ya usimamizi wa jopo la madaktari bingwa.

“Pacome Zouzoua anaendelea vizuri sana. Bado yupo hapa nchini na anahudhuria hospitali akitokea nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya vipimo na mazoezi maalum kulingana na maelekezo ya madaktari,” alisema Ali Kamwe.

Uongozi wa Yanga unasisitiza kuwa kwa sasa kipaumbele kikubwa ni kuhakikisha Mivoryian huyo anafuata kikamilifu kila hatua ya matibabu bila kuharakisha kurejea uwanjani, ili kulinda afya na kazi yake ya mpira wa miguu.

Pacome alipata jeraha hilo baya la mguu wakati wa mchezo wa kufungia msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League). Hata hivyo, taarifa hii ya maendeleo yake imewapa afueni na matumaini makubwa mashabiki wa Yanga wanaosubiri kwa hamu kumuona tena akiongoza safu ya ushambuliaji.

Kurejea kwa Pacome kwenye majukumu ya ushindani kutategemea zaidi tathmini ya mwisho kutoka kwa jopo la madaktari na jinsi mwili wake utakavyopokea hatua za mwisho za matibabu.

Record ya Simba vs Geita Gold Ligi Kuu Bara: Nani Kuibuka na Ushindi Meja Jenerali Isamuhyo? Rekodi Zinaibeba Yanga SC Dhidi ya Fountain Gate Arusha | Ligi Kuu Bara