Fountain Gate vs Yanga SC
Yanga SC

Rekodi Zinaibeba Yanga SC Dhidi ya Fountain Gate Arusha | Ligi Kuu Bara

Vardo August 30, 2026 4:05 pm

Kikosi cha Yanga SC kesho kitakuwa na kibarua kizito cha kusaka alama tatu muhimu kitakaposhuka dimbani kuwakabili wenyeji wao, Fountain Gate, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Mchezo huo uliokuwa umepangwa kuchezwa Jumanne, Septemba Mosi, umehesomeshwa mbele na sasa utachezwa kesho. Mabadiliko haya yanalenga kuipa Yanga muda wa kutosha wa kujiandaa na safari ya nchini Botswana, ambako itakabiliwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United.

Ubabe wa Yanga SC Mbele ya Fountain Gate

Yanga itaingia katika mchezo huu ikiwa na utulivu wa kisaikolojia kutokana na matokeo ya nyuma inapokutana na Fountain Gate, hususan katika mechi ambazo Fountain Gate inakuwa mwenyeji.

Takwimu za Ligi Kuu Bara zinaonyesha kuwa katika michezo minne iliyopita ambayo Fountain Gate imewakaribisha Wananchi, timu hiyo ya Arusha haijawahi kupata ushindi wala sare:

  • Msimu wa 2025/26: Fountain Gate 0–2 Yanga SC

  • Msimu wa 2024/25: Fountain Gate 0–4 Yanga SC

  • Msimu wa 2023/24: Fountain Gate 0–3 Yanga SC

  • Msimu wa 2022/23: Fountain Gate 0–2 Yanga SC

Katika mechi hizo nne, Wananchi wamevuna ushindi wa 100% huku wakifunga jumla ya mabao 11 bila kuruhusu lango lao kuguswa hata mara moja. Mchezo wa mwisho kuzikutanisha timu hizi kama mwenyeji ulichezwa Juni 18, 2026, ambapo Yanga iliondoka na ushindi wa mabao 2-0.

Licha ya takwimu hizi kuibeba Yanga SC, dakika 90 za uwanjani ndizo zitakazoamua kama Wananchi wataendeleza ubabe wao au Fountain Gate watavunja mwiko huo nyumbani.

Hali ya Pacome Zouzoua Yanga SC: Ali Kamwe Afunguka Maendeleo Yake Kiafya Mngqithi Aonya Yanga Dhidi ya Fountain Gate: “Hatuchukulii Mchezo Poa”