Simba vs Geita Gold
Simba SC

Record ya Simba vs Geita Gold Ligi Kuu Bara: Nani Kuibuka na Ushindi Meja Jenerali Isamuhyo?

Vardo August 30, 2026 3:49 pm

KIKOSI cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Steve Barker kinatarajiwa kushuka dimbani kesho Agosti 31, 2026, kuikabili Geita Gold katika mchezo mkali wa Ligi Kuu Bara utakochezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni.

Wekundu wa Msimbazi wanaingia kwenye pambano hili wakiwa na kiasi kikubwa cha kujiamini kutokana na historia nzuri waliyonayo dhidi ya wapinzani wao.

Rekodi ya Simba vs Geita Gold Kwenye Ligi Kuu Katika mikutano yao 6 iliyopita ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba haijapoteza mchezo hata mmoja dhidi ya Geita Gold:

  • Ushindi: Simba imeshinda mechi 5

  • Sare: Mechi 1

  • Mabao: Simba imefunga mabao 16 (wastani wa mabao 2.67 kwa mechi), huku Geita Gold ikifunga mabao 3 pekee (wastani wa bao 0.5 kwa mechi).

Historia ya Mechi zao Walizokutana:

  1. Msimu wa 2021/22: Simba ilishinda 2-1 nyumbani, kisha ikatoka sare ya 1-1 ugenini.

  2. Msimu wa 2022/23: Simba iliibuka na ushindi wa 3-0 nyumbani na kuifunga Geita Gold 5-0 ugenini.

  3. Msimu wa 2023/24: Simba ilipata ushindi wa 1-0 ugenini kabla ya kuhitimisha kwa ushindi wa 4-1 jijini Dar es Salaam (Mei 2024).

Je, Geita Gold Watavunja Mwiko? Pamoja na takwimu hizi kuibeba Simba SC, dakika 90 za uwanjani ndizo zitakazoamua. Geita Gold wanaingia katika mchezo huu wakisaka alama tatu muhimu na kujaribu kuvunja mwiko wa kutowahi kuifunga Simba tangu wapande Ligi Kuu.

Kwa upande wa Simba, ushindi ni lazima ili kuendeleza mbio zao za ubingwa na kuendeleza ubabe wao. Macho yote ya mashabiki wa soka nchini yatakuwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kushuhudia kama rekodi itaendelea au ukurasa mpya utaandikwa.

Mystery Multiplier Drop Inaleta Hadi X250 Ya Dau Lako Hali ya Pacome Zouzoua Yanga SC: Ali Kamwe Afunguka Maendeleo Yake Kiafya