Mtoto wa Jux na Priscilla
Burudani

Sura ya Mtoto wa Jux na Priscilla Yazua Mjadala Mzito Mitandaoni

Vardo August 30, 2026 4:20 pm

Siku tatu tangu mwanamuziki wa Bongo Flava, Juma Jux, na mkewe Priscilla Ojo (Priscy) waweke wazi sura ya mtoto wao, Prince Rakeem Mkambala, mjadala mpya umezuka kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii. Safari hii, mashabiki na wafuasi wao wanahoji: Mtoto huyo amefanana na nani zaidi?

Mjadala huo umeanza baada ya wazazi hao kumaliza mwaka mzima wakificha sura ya Rakeem. Kwa muda mrefu, walikuwa wakishiriki picha na video za maisha yake lakini kwa umakini mkubwa bila kuonyesha sura. Hakika, Priscy alishawahi kusisitiza kuwa angemwonyesha mwanaye pale muda sahihi utakapofika, badala ya kushinikizwa na matakwa ya mashabiki.

Hatimaye, mnamo Agosti 24, 2026, siku ambayo Rakeem alitimiza mwaka mmoja, wazazi wake waliamua kuvunja ukkimya na kuonyesha sura yake wazi kupitia picha za siku ya kuzaliwa.

Uamuzi huo ulipokelewa kwa furaha kubwa, lakini mara baada ya salamu za birthday kuisha, hisia tofauti zilianza kutawala maoni ya watu:

  • Upande wa Jux: Baadhi ya mashabiki wanaona Rakeem amebeba muundo wa uso wa baba yake, Jux, na kwamba ana baadhi ya sifa za dhahiri kutoka upande huo.

  • Upande wa Familia: Kundi jingine linadai mtoto huyo hafanani sana na Jux, bali amechukua sura ya mama mzazi wa msanii huyo (bi bibi yake).

  • Upande wa Ndudgu: Wapo pia wanaokwenda mbali zaidi na kudai Rakeem anafanana na mjomba wake, Mkambala JR (mdogo wa Jux).

Licha ya maoni hayo yote kushika kasi, hakuna kauli rasmi kutoka kwa familia ya Jux au Priscy inayothibitisha mtoto huyo amefanana zaidi na nani.

Kwa sasa, Rakeem akiwa bado ana umri wa mwaka mmoja pekee, ni wazi kuwa sura yake itaendelea kubadilika kadiri anavyokua. Mjadala unabaki kuwa wa mashabiki mitandaoni: Kwa mtazamo wako, Prince Rakeem amefanana na nani zaidi?

Mngqithi Aonya Yanga Dhidi ya Fountain Gate: “Hatuchukulii Mchezo Poa” Rekodi Mpya EPL: Mauzo ya Wachezaji Yanavyoingiza Mabilioni Msimu Huu