Simba SC

SIMBA SC YAFUZU ROBO FAINALI FA CUP KIBABE

admin May 1, 2021 6:29 pm

 


Mabingwa wa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania na kombe la FA , Simba SC imefanikiwa kuingia hatua ya  Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),  Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya  Kagera Sugara katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kagera Sugara walienda mapumziko wakiwa wanaongoza bao moja lililofungwa na Erick Mwijage dakika ya 45 kwa kichwa baada ya kupokea krosi ya beki Dickson Mhilu.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba SC, kufanya mabadiliko wakimtoa Taddeo Lwanga na nafasi yake ikichukuliwa na Bernard Morrison,kuingia kwa mchezaji huyu kulibadilisha mchezo na Simba kuanza kulisakama lango la Kagera Sugar kama nyuki.

Morrison aliwanyanyua mashabiki wa Simba SC dakika ya 55 akifunga goli la kusawazisha na dakika ya 67 Mshambuliaji  Meddie Kagere alifunga goli la pili .

Kwa matokeo hayo, Simba SC imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya FA Cup kwa msimu huu na kuweka hai matumaini ya kutetea taji la michuano hii ambalo walishinda msimu uliopita.

KIKOSI KAMILI CHA SIMBA SC DHIDI YA KAGERA SUGAR LEO DODOMA JIJI YAICHAPA KMC MABAO 2-0, YATINGA ROBO FAINALI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply