epl

TOTTENHAM YAMKOMALIA GARETH BALE

admin May 13, 2021 2:47 pm


KLABU ya Tottenham ina mpango wa kumuongezea muda wa mkopo kiungo mshambuliaji, Gareth Bale ambaye yupo hapo kwa mkopo akitokea kikosi cha Real Madrid.

Raia huyo wa Wales mkataba wake na Real Madrid unatarajiwa kufika tamati Juni 20, 2022.

Bale amekuwa akiweka wazi kwamba anahitaji kurejea katika timu yake hiyo ili aweze kupata changamoto tena chini ya Kocha Mkuu, Zinedine Zidane kwa kuwa ameshapata uzoefu.

Lengo la nyota huyo ni kwenda kumalizia mkataba wake katika timu yake tofauti na hapo alipo kwa sasa.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Daniel Levy anafanya jitihada kuhakikisha kwamba Bale anasalia kikosini hapo msimu wa 2021/22.

FEI TOTO APEWA NAMBA NDANI YA KIKOSI CHA SIMBA HARUNA NIYONZIMA ANAPATA TABU YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply