Yanga SC

KIKOSI CHA YANGA CHATINGA BUNGENI, DODOMA

admin May 18, 2021 10:47 am


 KIKOSI cha Yanga leo Mei 18 kimewasili salama makao makuu ya Tanzania, Dodoma na kupata fursa ya kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kuna vikao vya Bunge ambavyo vinaendelea.

Yanga ilianza safari leo Mei 18 asubuhi kuibukia Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania, unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, kesho Mei 19 majira ya saa 10:00 jioni.


Kupitia ukurasa wao rasmi wa Isntagram, Yanga waliandika namna hii:”Timu ya mabingwa wa kihistoria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”. 

KMC WAPEWA MAPUMZIKO YA SIKU 8 ISHU YA KANE KUSEPA SPURS BADO NGOMA NZITO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply