Simba SC

SIMBA YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA KUWAPA SAPOTI

admin May 26, 2021 2:47 pm


 BEKI wa Simba, Shomari Kapombe amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi leo Uwanja wa Mkapa kuwapa sapoti kwa kuwa wanaamini watapambana ili kupata ushindi.

Simba wataingia kwenye mchezo wa leo wakiwa ni mabingwa watetezi wa taji hilo na wanakumbuka kwamba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wameishia hatua ya robo fainali na lengo lao la kutinga hatua ya nusu fainali limekwama.

Kapombe alikuwa ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes hivyo huenda leo akiwa fiti anaweza kuanza pia.


Ni mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali ambapo mshindi wa leo atakutana na mshindi wa mchezo wa Rhino Rangers v Azam FC.

Kapombe amesema:”Tupo tayari kwa ajili ya ushindani na maandalizi yapo vizuri, kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwa kuwa tunahitaji ushindi.

“Sisi ni wao na wao ni sisi, hivyo tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi, Uwanja wa Mkapa,”.

Kwa upande wa mkata umeme, Taddeo Lwanga amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi nao kuwapa sapoti. 

Mchezo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku, Uwanja wa Mkapa. Tayari watani zao wa jadi Yanga wamekata tiketi ya kushiriki nusu fainali ambapo watacheza na Biashara United, Tabora, Uwanja wa Al Hassan.

TRY AGAIN : MSIMU UJAO SIMBA SC TUTAKUWA NA KIKOSI BORA ZAIDI KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA DODOMA JIJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply