news

WAZIRI NDUMBARO AMPA ZAWADI NYOTA WA CRYSTAL PALACE, AAHIDI KUWALETA MASTAA BONGO

admin June 1, 2021 1:47 pm


 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt Damas Ndumbaro amepa zawadi ya moja ya kikombe chenye nembo ya Hifadhi za Taifa, nyota wa Klabu ya Crystal Palace na timu ya Taifa ya Ufaransa, Mamadou Sakho.


Nyota huyo ameambata na mkewe Majda Sakho ambapo hayo yalitokea mara baada ya mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Jijini Dodoma.


Nyota huyo ameahidi kuwaleta mastaa wengi wa soka kuja kutembelea vivutio vya utalii nchini.


Ikumbukwe kuwa Mamadou Sakho ni Balozi wa Hiari wa Utalii Tanzania ameongeza kwa kusema kuwa amekuwa akiulizwa kuhusu madhari na uzuri wa eneo ambazo amekuwa akizitangaza kupitia mitandao ya kijamii.

“Nimekuwa nikiulizwa kuhusu mazingira ambayo ninapigia picha hasa pale ninapoziweka kwenye mitandao ya kijamii. Ninapenda kuona namna hali ilivyo pamoja na ukarimu nilioupata.
“Imani yangu ni kwamba nitaleta mastaa wengi zaidi hapa ili kuweza kuona zaidi uzuri wa maneo ya Tanzania,” .
MORRIS: BADO TUNA KAZI KUBWA YA KUFANYA KUMBE CARLINHOS ALIPUUZIA PROGRAMU ALIYOPEWA NA MADAKTARI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply