Yanga SC

YANGA BADO INAPIGIA HESABU UBINGWA

admin June 1, 2021 12:47 pm


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa bado una matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara uliopo mikononi mwa Simba.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili ina pointi 61 huku watani zao wa jadi wakiwa nafasi ya kwanza na pointi zao 64.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa bado watazidi kupambana mpaka tone la mwisho kufikia malengo ambayo wameweka.

“Kikubwa ni kwamba tupo kwenye ushindani nasi tunapambana kupata matokeo mazuri, jambo la msingi ni kuona tunazidi kushirikiana na kuwa pamoja.

“Mashabiki waendelee kutupa sapoti ili kuona tunapata matokeo chanya, bado uwezo upo na nia ipo hivyo kazi inaendelea mpaka tone la mwisho,” .

Simba inatetea taji hilo ambalo ilitwaa msimu uliopita na iliweza kutinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

SIMBA WATUA MWANZA KAMILI KUWAVAA RUVU SHOOTING AME AKINGIWA KIFUA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply