News

MASAU BWIRE: TUTAWAFUNGA SIMBA KESHO

admin June 2, 2021 6:47 pm


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa kesho wanauhakika wa kuwapapasa wapinzani wao Simba iki kubadili wimbo kwa kila Mtanzania.

Ruvu Shooting itawakaribisha wapinzani wao Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Juni 3.

Katika mchezo wao wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma Simba 0-1 Ruvu Shooting hivyo kesho wanahitaji kulinda rekodi yao na Simba wao wanawaza kulipa kisasi.

Masau amesema:”Hamna namna tunataka kuwafunga Simba ili kuonyesha kwamba nasi tupo imara, suala la wao kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika hiyo haitutishi tutafanya vizuri na tupo imara,” .

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara,  Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 na pointi 37 huku Simba ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 64.

USIPANGE KUKOSA NAKALA YAKO JERO TU GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply