Jina la Ibrahimu Ajibu lilikuwa miongoni mwa wachezaji wazawa waliojadiliwa katika moja ya vikao vya makati ya usajili wa Yanga, lakini kamati hiyo imeeleza sababu za kutoafikiana juu ya usajili huo.
Mmoja wa vigogo wa kamati ya usajili ya Yanga aliyeomba hifadhi ya jina alisema baada ya jina la Ajibu kupelekwa mezani kwao, hawakutaka kupepesa macho.
“Ni kweli baadhi yetu walimpendekeza, lakini wengi tulimkataa kwa sababu,” alisema kigogo huyo wa usajili wa Yanga aliyeomba hifadhi ya jina.
Alisema kilichomuondoa Ajibu katika rada za usajili wa Yanga ni kuonekana hatokuwa na kipya kuisaidia timu hiyo.
“Ajibu sio mchezaji mbaya, lakini inaonekana ameridhika na hatua aliyopo, hivyo alipopendekezwa arudi Yanga, fasta kuna baadhi ya wajumbe walimkataa pale pale bila kupepesa macho,” amesema mjumbe huyo.