Simba SC

KOCHA BARKER AWEKA WAZI MBEYA CITY SIO WAPINZANI WEPESI

Vardo June 16, 2026 9:30 pm

KOCHA Mkuu wa Simba, Steven Barker, ameweka wazi kuwa kikosi chake kimejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, akisisitiza kuwa hakuna timu ya kudharau katika hatua hii ya msimu.

Barker amesema licha ya Simba kuwa na nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi ukilinganisha na wapinzani wao, hilo halibadilishi ukubwa wa changamoto inayowakabili dhidi ya Mbeya City ambao wanapambana kuhakikisha wanabaki salama kwenye ligi kuu.

Amefafanua kuwa michezo ya mwisho wa msimu huwa na presha na ushindani mkubwa, kwani kila timu huingia uwanjani ikiwa na malengo tofauti lakini yenye uzito sawa wa kutafuta matokeo chanya.

Kocha huyo amesisitiza kuwa mechi dhidi ya timu zinazopigania maisha yao kwenye ligi huwa ngumu zaidi, kwa sababu zinacheza kwa nguvu, ari na nidhamu kubwa ya kupambana hadi dakika ya mwisho.

“Hatuwadharau wapinzani wetu. Kila timu kwa sasa ina malengo yake na unapocheza dhidi ya timu inayopambania kubaki ligi kuu, unapaswa kuwa makini zaidi kwa sababu mechi inakuwa ngumu,” amesema Barker.

Ameongeza kuwa Simba inahitaji kuingia uwanjani ikiwa imejipanga kiakili na kimkakati, huku ikitambua umuhimu wa kupata matokeo chanya katika kila mchezo uliosalia wa msimu.

Amesema maandalizi yao yanaendelea vizuri na wachezaji wako katika hali nzuri ya kisaikolojia na kimwili kuelekea mtanange huo unaotarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa.

BEKI WA CHELSEA SHAVU ZITO KOMBE LA DUNIA DAKIKA ZA JIONI KWA GOAL STRIKE FRENZY KILA MCHEZO UNAKUWA USHINDI MKUBWA