Afrika Kusini vs Ivory Coast WAFCON
Habari za michezo

Afrika Kusini Yaamka Kiumeni na Kulazimisha Sare ya 2-2 Dhidi ya Ivory Coast

Vardo August 1, 2026 11:36 am

Afrika Kusini Yaamka Kiumeni na Kulazimisha Sare ya 2-2 Dhidi ya Ivory Coast

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) imeonyesha ujasiri mkubwa baada ya kutoka nyuma kwa mabao mabao mawili na kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Ivory Coast kwenye mchezo wa Kundi B wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) uliopigwa katika Uwanja wa Rabat Olympic.

Sare hiyo inakuwa matokeo ya pili kwa timu zote mbili katika hatua ya makundi. Banyana Banyana iliingia uwanjani ikitaka kujirekebisha baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania, huku Ivory Coast ikitoka kwenye ushindi mnene wa 4-1 dhidi ya Burkina Faso.

Ivory Coast Yatawala Kipindi cha Kwanza

Ivory Coast ilianza mchezo huo kwa kasi na kulifanya lango la Afrika Kusini kuwa kwenye shinikizo kubwa. Grace Sery ndiye aliyekuwa mwiba kwa Banyana Banyana baada ya kufunga mabao yote mawili ya Ivory Coast katika dakika ya 18 na 36, na kuifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Hadi kipindi cha kwanza kinatamatika, Ivory Coast ilionekana kutawala kila idara kuanzia umiliki wa mpira, upigaji wa pasi sahihi pamoja na mashuti yaliyolenga lango. Takwimu za mwisho wa mchezo zinaonyesha Ivory Coast ilimiliki mpira kwa asilimia 63.5 dhidi ya 33.5 za Afrika Kusini, huku ikipiga mashuti 11 yaliyolenga lango dhidi ya mashuti 2 pekee ya Banyana Banyana.

Banyana Banyana Yarudi Kivingine Kipindi cha Pili

Kipindi cha pili kilileta sura mpya kwa mabingwa hao watetezi. Afrika Kusini iliongeza kasi na kupambana kurudisha mabao hayo. Dakika ya 71, mshambuliaji nyota Thembi Kgatlana alifunga bao la kwanza la Banyana Banyana na kupunguza tofauti ya mabao.

Wakati mchezo ukinyemelea ukingoni, Hildah Magaia alikuwa shujaa wa Afrika Kusini baada ya kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya 90 na kuipa timu yake pointi ya kwanza muhimu katika kundi hilo.

Msimamo wa Kundi B

Matokeo hayo yanaifanya Ivory Coast kuendelea kushikilia usukani wa Kundi B ikiwa na pointi nne (4) baada ya michezo miwili.

  • Ivory Coast: Pointi 4 (Michezo 2)

  • Tanzania: Pointi 3 (Mchezo 1)

  • Afrika Kusini: Pointi 1 (Michezo 2)

  • Burkina Faso: Pointi 0 (Mchezo 1)

Yanga Yakamilisha Dili la Fred Ngoma Kutoka Morocco | Dau Milioni 662! Hesabu za Twiga Stars WAFCON 2026: Jinsi Tanzania Inavyoweza Kufuzu Robo Fainali