Simba vs Azam 2-0
Simba SC

Simba Yaifunga Azam FC 2-0 Mzizima Derby: Rushine De Reuk na Chama Waiteka Chamazi

Vardo September 17, 2026 10:30 am

Simba SC imefanikiwa kufuta uteja dhidi ya Azam FC baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 2-0 katika mchezo wa Mzizima Derby uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulianza kwa kasi kubwa, ambapo wenyej wao Azam FC walipata nafasi ya mapema dakika ya 11 kupitia kwa Elie Mpanzu. Hata hivyo, shuti lake lilipita nje kidogo ya lango la Simba na kuwafanya kukosa nafasi hiyo muhimu. Kipindi cha kwanza kiliendelea kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku safu za ulinzi zikisimama imara na kufanya dakika 45 za kwanza kumalizika bila kufungana.

Kipindi cha pili kilitawaliwa na mabadiliko ya mbinu kwa upande wa Simba SC. Kasi yao mpya ilizaa matunda dakika ya 59 pale Rushine De Reuk alipopachika bao la kwanza na kuifanya Simba kushika hatamu za mchezo.

Kabla ya Azam FC kujipanga upya, kiungo mshambuliaji Clatous Chama aligongilia msumari wa pili dakika ya 67, akionyesha ubora wake na kuipa Simba ushindi wa mabao 2-0 pamoja na pointi tatu muhimu.

Ushindi huu umekuwa na maana kubwa kwa Simba SC, kwani si tu kwamba umeondoa uteja wa msimu uliopita ambapo waliambulia pointi moja pekee dhidi ya Azam FC, bali pia umeongeza ushindani mkali kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu. Hivi sasa Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 18, sawa na viongozi wa ligi hiyo Yanga SC.

Yanga Kukipiga na St. George Dar es Salaam: Maandalizi Yaiva Uwanja wa Uhuru! Ibenge Afunguka Sababu za Azam FC Kukung’utwa na Simba Mzizima Derby