Rushine De Reuck Simba SC
Simba SC

De Reuck Afichua Siri ya Simba Kuichapa Azam FC 2-0 Mzizima Derby

Vardo September 17, 2026 10:49 am

Nahodha wa Simba SC, Rushine De Reuck, ameweka wazi kuwa ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa Mzizima Derby haukuwa wa bahati mbaya, bali ni matokeo ya nidhamu kubwa, kujituma, na kupambana hadi dakika ya mwisho.

Simba iliibuka na ushindi huo muhimu katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, ambapo De Reuck mwenyewe alipachika bao la kwanza kabla ya kiungo mshambuliaji Clatous Chama kufunga bao la pili na kuhakikisha pointi zote tatu zinakwenda Msimbazi.

“Nidhamu na Juhudi Zilitupa Ushindi”

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa pambano hilo, De Reuck alisema benchi la ufundi na wachezaji walitambua mapema ubora wa Azam FC, hivyo waliingia uwanjani wakiwa wamejiandaa kupambana kwa nguvu zote.

“Haikuwa mechi rahisi kwa sababu tulikuwa tunacheza dhidi ya timu nzuri. Tulijua kabla ya mchezo kwamba tungehitaji juhudi kubwa na kujitoa, na nadhani vijana walionyesha hilo leo,” alisema De Reuck.

“Kila Mechi ni Vita Kwetu”

Licha ya Simba kuendelea na mwenendo mzuri wa matokeo msimu hii, nahodha huyo alisisitiza kuwa hakuna mchezo mwepesi kwenye ligi na wamekuwa wakipigania kila pointi kwa jasho na damu.

“Haijawa rahisi kwetu. Michezo yote ambayo tumekuwa tukishinda hadi sasa haikuwa rahisi, lakini timu imeendelea kupambana na kuonyesha kujituma. Najivunia sana kuwa sehemu ya timu hii na, bila shaka, kuwa nahodha wake.”

Ujumbe Mzito kwa Mashabiki wa Simba

De Reuck hakusita kuwasifu mashabiki wa Simba kwa kujitokeza kwa wingi na kutoa hamasa kubwa iliyowapa nguvu wachezaji uwanjani, huku akiwaomba waendelee kuwasimamia hata nyakati ngumu.

“Mashabiki wanabadilisha hali ya mambo na kukupa hamasa ya kufanya kila kitu uwanjani. Wao ni motisha kubwa kwetu. Tunawashukuru kwa sapoti na tunawaomba waendelee kuwa nasi wakati wa mazuri na mabaya, kwa sababu kwenye soka huwezi kushinda kila mchezo.”

Barker Ataiwezesha Simba Kuichapa Yanga Kariakoo Derby? Ahmed Ally Aivulia Kofia Kalenda ya FIFA, Awaonya Yanga Elekea Kariakoo Derby