Taifa Stars

ISRAEL MWENDA AMTAJA ALIYEMWAMBIA APIGE PIGO HURU LILILOWAMALIZA WAMALAWI

admin June 14, 2021 5:48 am


NYOTA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Israel Mwenda amesema kuwa aliambiwa apige pigo huru na Mohamed Hussein ambaye wanacheza naye.

Jana, Juni 13 kwenye Uwanja wa Mkapa, Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malawi ambapo watupiaji walikuwa ni John Bocco ambaye ni nahodha pamoja na Mwenda ambaye alipachika bao la pili kwa pigo huru akiwa nje ya 18. 

Mwenda amesema:” Mohamed Hussein aliniambia nipige ile Free Kick( pigo huru) ndio maana nilipiga. Huwa nafanya mazoezi sana ya free kick ndio maana huwa nafunga mabao ya namna hiyo.

“Namshukuru Mungu na najiskia faraja kwa kucheza na kuiwakilisha nchi yangu, pia kuweza kufunga katika mchezo jambo hili litakaa katika kumbukumbu za maisha yangu yote.

Mchezo huo ulikuwa ni wa kirafiki ambao upo kwenye kalenda ya Fifa ulihudhuriwa na mashabiki wengi ambao walijitokeza kuipa sapoti Stars.

UKRAINE WAPEWA ONYO ISHU YA ULINZI BAADA YA KUPOTEZA KATIKA EURO 2020 MTIBWA SUGAR YAINYOOSHA TANZANIA PRISONS, AZAM V KAGERA YAWEKA REKODI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply