news

MALALE HAMSINI ATAJA SABABU YA KUSHINDWA KUSHINDA MBELE YA SIMBA

admin June 20, 2021 4:47 pm


 MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa walishindwa kupata matokeo mbele ya Simba kwa kuwa wachezaji wake walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata.

Jana, Juni 19 ikiwa Uwanja wa CCM Kirumba ilikubali kupoteza pointi tatu baada ya ubao wa uwanja huo kusoma Polisi Tanzania 0-1 Simba.

Alikuwa ni Luis Miqussone ambaye alipachika bao akiwa nje ya 18 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Mohamed Yusuf wa Polisi Tanzania.

Malale amesema:”Haikuwa kazi rahisi kwetu kuweza kushinda kutokana na wachezaji wangu kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata.

“Kuna wakati walipata nafasi ya kufunga ila walishindwa lakini kwa kuwa imetokea basi huwezi kubadili matokeo ambayo yametokea ni wakati wetu kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo,” amesema.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 2-0 Polisi Tanzania.

Ndani ya dakika 180 Polisi Tazania imefungwa jumla ya mabao matatu huku safu yao ya ushambuliaji ikiwa haijafunga mbele ya Simba. 

Tayari kikosi cha Simba kimeshawasili Dar leo Juni 20 baada ya kusepa na pointi tatu za Polisi Tanzania.

KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA MWADUI FC VIDEO: NAMNA KIKOSI CHA YANGA KILIVYOWASILI UWANJA WA MKAPA, DAR

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply