Simba SC

SIMBA YAPOKELEWA NA NYOMI YA MASHABIKI SONGEA

admin June 23, 2021 12:47 pm


MASHABIKI wa Simba leo wamejitokeza kwa wingi kuipokea timu hiyo ambayo imewasili leo Juni 23, Songea.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majimaji, Juni 26.

Ni Simba ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo walitwaa msimu uliopita baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC ilikuwa Uwanja wa Nelson Mandela.

Gomes amesema:”Tunatambua kwamba Azam FC ni timu bora kwani ina wachezaji wazuri hivyo wachezaji wangu nimewaambia kwamba wanapaswa kufanya kazi kwa umakini kusaka ushindi,” .


ISHU YA LAMINE, MNATA NA SAIDO BADO NI TATIZO KWA YANGA SIMBA YAWAOMBA WAKAZI WA SONGEA KUWAPA SAPOTI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply