Simba SC

SIMBA YAWAOMBA WAKAZI WA SONGEA KUWAPA SAPOTI

admin June 23, 2021 1:47 pm


ERASTO Nyoni kiraka ndani ya kikosi cha Simba amesema kuwa wanaimani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majimaji, Songea Juni 26 na leo Juni 23 kikosi kimeibukia Songea na kupokewa na mashabiki wao.

Mshindi wa mchezo huo atakutana na Yanga ama Biashara United ambao wao watacheza nusu fainali Juni 25.

Nyoni amesema:”Wakazi wa Songea wajitokeze kwa wingi kutupokea kwa kuwa tunakwenda kwenye mchezo wetu mgumu na utakaokuwa na ushindani mkubwa.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo na hilo lipo wazi hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema Nyoni.

Simba ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji katika chezo wa robo fainali uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

SIMBA YAPOKELEWA NA NYOMI YA MASHABIKI SONGEA COASTAL UNION MAMBO BADO, MGUNDA KUBEBA LAWAMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply