Michael Carrick kutimuliwa Man United
Habari za michezo

Michael Carrick Matatani Man United: Eddie Howe Kutajwa Kuchukua Mikoba

Vardo August 25, 2026 8:26 pm

MANCHESTER, England — Kocha wa Manchester United, Michael Carrick, ameingia kwenye shinikizo kubwa baada ya kuongopea masoko ya ubashiri kuwa kocha aliye hatarini zaidi kutimuliwa kazi kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) msimu huu.

Shinikizo hilo limeongezeka kufuatia kipigo cha kusikitisha cha mabao 2-0 walichokipata Manchester United dhidi ya Hull City Siku ya Jumamosi. Licha ya Man United kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa, kikosi cha Carrick kilionyesha kiwango duni katika maeneo yote ya uwanja na kushindwa kuipenya safu ya ulinzi ya wageni hao wapya Ligi Kuu.

Kipigo hicho kimezua maswali magumu kuhusu mustakabali wa Carrick Old Trafford, hasa ikizingatiwa kuwa mashabiki na uongozi walikuwa na matumaini makubwa kuelekea msimu huu kufuatia usajili wa wachezaji wapya na maandalizi mazuri ya msimu.

Odds za Carrick Kutimuliwa Zashuka Kasi

Kampuni ya ubashiri ya Betfair imeshusha odds za Carrick kuwa kocha wa kwanza kutimuliwa kutoka 33/1 hadi 6/1, hatua iliyomfanya ashike nafasi ya kwanza kwenye soko la makocha walio hatarini.

Kwa sasa, Carrick amewapita makocha wengine kama Sergej Jakirović na Frank Lampard ambao wote wana odds za 7/1.

Orodha ya Makocha Walio Hatarini Kutimuliwa EPL:

  • Michael Carrick – 6/1 (Kutoka 33/1)

  • Sergej Jakirović – 7/1

  • Frank Lampard – 7/1

  • Roberto De Zerbi – 17/2

  • Álvaro Arbeloa – 17/2

  • Gary O’Neil – 9/1

  • Oliver Glasner – 9/1

  • Enzo Maresca – 12/1

  • Unai Emery – 12/1

  • Matthias Jaissle – 12/1

  • Régis Le Bris – 12/1

  • Pierre Sage – 16/1


Eddie Howe Asewa Kuwa Chaguo la Kwanza Kutua Old Trafford

Wakati hali ikiwa mbaya kwa Carrick, aliyekuwa kocha wa Newcastle United, Eddie Howe, ameibuka kama mwalimu anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kuchukua mikoba ya kuifundisha Manchester United endapo Carrick ataonyeshwa mlango wa kutokea.

Howe, ambaye aliondoka Newcastle majira ya joto yaliyopita na kuamua kupumzika, anapewa nafasi ya kwanza kwenye masoko ya ubashiri. Makocha wengine wanaotajwa kufuatilia kiti hicho ni pamoja na Julian Nagelsmann (odds za 10/3) na Thomas Tuchel (odds za 4/1).

Kocha Josiah Aifungia Kazi Mashujaa FC Kuelekea Dhidi ya Kagera Sugar Timu 6 Zilizokwama Dakika 270 Ligi Kuu Bara 2026: Presha Ya Kushuka Daraja Yaanza Mapema!