FA Cup

NYOTA HAWA SITA WA YANGA KUIKOSA BIASHARA UNITED LEO

admin June 25, 2021 6:47 am


WAKATI leo kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi kikitarajiwa kushuka Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United nyota wake sita itawakosa.

Mchezo wa leo ni wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho  na mshindi wa leo atacheza fainali na mshindi wa mchezo kati ya Azam FC na Simba utakaochezwa kesho, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Nyota hao ni pamoja na Lamine Moro, Michael Sarpong, Metacha Mnata hawa kutokana na masuala ya nidhamu ndani ya kikosi hicho.

Mapinduzi Balama, Yassin Mustapha na Abdalah Shaibu, ‘Ninja’ hawa bado hawajawa fiti kutokana na kutibu majeraha yao.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhamasihaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa Balama, Ninja maendeleo yao ni mazuri.

UEFA YAFUTA SHERIA YA BAO LA UGENINI VIDEO: TFF YAMFUNGULIA MWAKALEBELA, YANGA KUISAKA FAINALI LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply