epl

RAHEEM AIGOMEA CITY KUWA CHAMBO

admin June 24, 2021 4:47 am


MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Raheem Sterling hana mpango wa kuondoka hapo ili timu hiyo iweze kupata saini ya mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane.

Imekuwa ikielezwa kuwa City ina mpango wa kupata saini ya Kane huku ikiwaweka chambo baadhi ya wachezaji wake na inatajwa kuwa Sterling ni mmoja wapo.

Mkwanja ambao City inayonolewa na Pep Guardiola wametenga mezani ni milioni 100 pauni ila zimekataliwa na bosi wa Tottenham, Daniel Levy ambaye anataka zaidi ya fedha hizo jambo ambalo limewafanya City kuwa na mpango wa kuwapa wachezaji wawili.

Taarifa zinasema kuwa Sterling amegomea kutolewa kwa mpango huo na ikiwa ataondoka ndani ya kikosi hicho itakuwa ni kwa mpango wake binafsi na sio wa timu kumtoa chambo ili wampate mchezaji.

NYOTA HAWA 7 WATAJWA KUINGIA ANGA ZA YANGA ILI WAMWAGE SAINI MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply