Simba SC

GOMES – MATOKEO YA JUMAMOSI YAMETUUMIZA MNO

admin July 5, 2021 3:47 pm


Baada ya kupoteza mchezo wa jumamosi dhidi ya Yanga, Kocha Mkuu Didier Gomes amesema matokeo hayo yametuumiza kwani tumewaangusha mashabiki wetu ambao walikuwa na matumaini makubwa.

Gomes amesema tulipaswa kushinda kwenye mchezo mkubwa na kutawazwa mabingwa wa ligi lakini haikutokea hivyo yeye kama kocha mkuu anapaswa kubeba jukumu hilo.

Raia huyo wa Ufaransa amesema hatukucheza vizuri hasa kipindi cha kwanza na tulipoteza pasi na kuruhusu kushambuliwa zaidi kitu ambacho hatukutarajia kutokea.

β€œNi matokeo ambayo hatukuyategemea yametuumiza na tumewaangusha mashabiki wetu. Tulistahili kushinda kwenye mechi kubwa ili kutawazwa mabingwa lakini haikutokea.

β€œHatukucheza vizuri kipindi cha kwanza lakini cha pili tulikuwa bora na tulitengeneza nafasi za kufunga lakini hatukuwa na bahati,” amesema Gomes.

AZAM FC ILE YA NUSU FAINALI IJITAFUTE MUDA WOTE VIGONGO VYA SIMBA BONGO ACHA KABISA, YANGA NDANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply