Simba SC

GOMES AWAWASHIA TAA YA KIJANI NDEMLA NA GADIEL MICHAEL

admin July 8, 2021 12:16 pm


Baada ya kujihakikishia kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mara ya nne mfululizo Kocha Mkuu, Didier Gomes amesema atawapumzisha baadhi ya wachezaji waliotumika sana na kuwapa nafasi wengine.

Gomes amewataja nyota hao Miraji Athuman, Said Ndemla, Gadiel Michael na David Kameta kuwa wanafanya vizuri mazoezini na anafurahi kufanya nao kazi lakini kutokana na ukubwa wa kikosi wameshindwa kupata nafasi.

Gomes amesema msimu ulikuwa mrefu na wachezaji walipambana na kufanikisha tunatetea ubingwa hivyo kwenye mechi tatu za ligi zilizosalia atawapa nafasi nyota wengine ambao hawajacheza mara nyingi.

โ€œTunashukuru tumefanikiwa kutetea ubingwa wetu, nadhani tutawapumzisha wachezaji waliocheza mechi nyingi na kuwapa nafasi wengine sababu msimu ulikuwa mrefu.

โ€œKatika mechi tatu za ligi zilizobaki tutawapa nafasi wachezaji ambao hatukuwatumia sana. Simba ni familia ukipanga kikosi bado unakuwa na wachezaji 10 ambao ni bora lakini wanakosa nafasi hivyo ni wakati wao huu,โ€ amesema Gomes.

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata jana dhidi ya KMC tumejihakikishia kutetea ubingwa kufuatia kufikisha alama 76 ambazo zinaweza kufikiwa na anayetufuatia lakini tumemzidi uwiano wa mabao ya kufunga.

KATUMBI AWATIBULIA YANGA DILI LA KIUNGO MKONGO..AMWAGA MAMILIONI SAMATTA – YANGA WAMSHUKURU MORRISON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply