Simba SC

MWENDA AMKIMBIZA BEKI SIMBA

admin July 24, 2021 4:43 pm


MLINZI wa kulia wa klabu ya Simba, David Kameta ‘Duchu’ huenda akawa sehemu ya kikosi cha klabu ya Mbeya kwanza kitakachoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao kama mchezaji wa mkopo akitokea Simba.

Duchu alisajiliwa na Simba kutokea klabu ya Lipuli mwanzoni mwa msimu huu, lakini amekuwa katika wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza mbele ya beki Mwandamizi, Shomari Kapombe.

Uamuzi huo wa kumtoa kwa mkopo Duchu unatokana na usajili wa mlinzi wa kulia, Israel Patrick Mwenda ambaye taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza kuwa tayari amesaini mkataba wa miaka mitatu.

JEMBE JIPYA LAWEKA WAZI SABABU ZA KUMWAGA WINO AZAM SIMBA WAKOMAA NA BANDA WA MALAWI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply