news

AMISS TAMBWE KURUDI BONGO ISHU IPO HIVI

admin August 2, 2021 11:43 am

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Klabu ya Yanga, Amis Tambwe amesema kuwa yupo tayari kurudi Bongo ikiwa itatokea timu inamuhitaji ili aweze kusaini.
Tambwe anakumbukwa na mashabiki wa Yanga kutokana na uwezo wake wa kucheka na nyavu ambapo alisepa Tanzania msimu wa 2018/19 kutokana na mkataba wake kuisha.
Alifunga mabao 8 kwenye ligi na manne kwenye Kombe la Shirikisho na kumfanya afunge jumla ya mabao 12 ndani ya Yanga wakati akisepa.
Tambwe amesema kuwa kwa sasa yupo Burundi akiwa huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu aliyokuwa anacheza nchini Djibout.
“Nipo kwa sasa nyumbani kwa kuwa nilirudi baada ya kumaliza mkataba wangu nilipokuwa nacheza Djibouti la ikitokea timu Tanzania ninaweza kusaini kwani mpira ni kazi yangu,” amesema Tambwe.

NAMUNGO FC KUPITISHA PANGA KWA NYOTA 7, ORODHA HII HAPA, SALAMBA NDANI VIDEO:ALIYEITUNGUA YANGA ATAJA HESABU ZAO MECHI ZA MBELE KAGAME

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply