Yanga SC

YANGA YAINGIA ANGA ZA RASTA WA POLISI TANZANIA

admin August 3, 2021 9:43 pm


 KIUNGO wa Polisi Tanzania, Hassan Nassoro inaelezwa amemalizana na mabosi wa Yanga kwa ajili ya kuwatumikia kwa msimu ujao.

Nassoro mwenye rasta kichwani amekuwa na msimu mzuri ndani ya uwanja licha ya jina lake kuwekwa kwenye orodha ya wale waliomaliza mkataba na hawataongeza mkataba.

Mtu wa karibu wa Nassoro amesema kuwa mabosi wa Yanga wamefanya mazungumzo na Nassoro hivyo ni suala la muda kufikia makubaliano ya kusaini dili jipya.

“Nassoro kwa sasa yupo huru kujiunga na timu ambayo itafikia dau la kumpa kandarasi mpya lakini Yanga wameonekana kuwa karibu kumpa mkataba hivyo ni suala la kusubiri,” ilieleza taarifa hiyo.

Alipotafutwa Nassoro alisema kuwa bado kwa sasa hajapata taarifa kuhusu kujiunga na Yanga.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga katika Kamati ya Mashindano amesema kuwa mipango ya usajili ipo na wanaamini watafanya mambo hayo kwa umakini.

Tayari Yanga imemsajili Yusuph Athuman, Fiston Mayele na Heritier Makambo na wameweka wazi kwamba kazi inaendelea.



NAHODHA WA ASTON VILLA AREJEA KIKOSINI LUIS MIQUISSONE HUYO KUIBUKIA KWA WAARABU, DILI LAKE MIAKA MINNE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply