Yanga SC

NI UWONGO..ISHU YA KISINDA KWENDA MOROCCO IKO HIVI KUMBE..

admin August 10, 2021 3:47 pm


Imefahamika kuwa picha inayoendelea kusambaa kwa kasi ikimuonesha kiungo mshambuliaji kutoka DR Congo na klabu ya Young Africans Tuisila Kisinda akiwa na viongozi wa RS Berkane imefanyiwa uhariri (Editing).

Kisinda anayehusishwa na usajili ndani klabu hiyo ya Morocco, bado ni mchezaji halali wa Young Africans, licha kuwepo kwa taarifa za kuwa mbioni kuondoka katika kipindi hiki.

Picha inayoendelea kusambaa imemuonesha kiungo huyo kutoka DR Congo akitambulishwa huku akiwa ameshika jezi ya klabu ya RS Berneke inayonolewa na Kocha Florent Ibenge ambaye aliwahi kufanya kazi na Kisinda kwenye klabu ya AS Vita ya mjini Kinshasa.

Katika hatua nyingine Uongozi wa Young Africans kupitia kwa Eng. Hersi Said umethibitisha kuwa wamepokea Ofa kutoka klabu ya RS Berkane inayomhitaji Tuisila Kisinda mwenye umri wa miaka 21.

Hersi ameongeza kuwa pia wamepokea ofa zinazohusu wachezaji wao wengine kama Yacouba Songne na Mukoko Tonombe.

Mpaka sasa dili la Kisinda ndilo linaloonekana kuwa na nguvu zaidi na muda wowote winga huyo atatua Morocco kwa ajili ya kukamilisha uhamisho huo.

MESSI AKUBALI KUSAINI MIAKA MIWILI, PICHA YAKE YAONDOLEWA BAADA YA KUTEMANA NA MESSI, BARCELONA WAIPELEKA PSG MAHAKAMANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply