News

BAADA YA KUTEMWA AS VITA…PILAU NA BIRIAN VYAMRUDISHA TSHISHIMBI BONGO

admin August 21, 2021 5:30 pm


NAHODHA wa zamani wa Yanga, Papy Tshishimbi amethibitisha mapenzi yake na Tanzania baada ya kurudi tena kula maisha baada ya kumaliza mkataba na AS Vita.

Tshishimbi alishawahi kulithibitishia Soka la Bongo Blog kuwa anaipenda Tanzania na anatamani kubadili uraia wake kutoka DR Congo na kuwa Mtanzania.

Amesema yupo Tanzania kwaajili ya maisha yake binafsi na sio jambo lolote linalohusu soka na kubainisha kuwa ameamua kuachana na soka.

“Nipo nchini hapa lakini hakuna ishu yoyote iliyonileta kuhusu mpira nimekuja tu kutembea kwasababu ni nchi ambayo naipenda na nilikaa kwa muda mrefu na kupewa ushirikiano mzuri,” alisema.

Awali akihojiwa na moja ya chombo cha habari, Tshishimbi alifunguka kuwa mbali na mazingira ya Tanzania, pia anapenda sana vyakula vinavyopikwa hapa, ikiwemo biriani na pilau, hivyo pengine pia hii ikawa sababu ya kumfanya kurudi nchini.

PAMOJA NA KUAGA MSIMBAZI…CHAMA AFUNGUKA HAYA KUHUSU MO DEWJI NA BARBARA PAPE SAKHO AANZA KWA KASI YA 5G SIMBA …APIGA GOLI LA KIULAYA ULAYA MECHI IKIISHA KWA SARE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply