Yanga SC

BAADA YA KUMKIMBIA SVEN MOROCCO…LITOMBO ATOA KAULI YA KIBABE YANGA

admin August 22, 2021 3:43 pm


BEKI wa kati wa Yanga, Yanick Bangala Litombo amesema kuwa anasubiri kwa hamu kuanza kuitumikia klabu yake mpya ya Yanga tayari kwa msimu ujao katika mashindano mbalimbali ambayo timu hiyo itashiriki.

Litombo hivi karibuni aliachana na klabu ya Far Rabat ya nchini Morocco inayonolewa na kocha wa zamani wa Simba, Sven Vandenbroeck kwa kuvunja mkataba na klabu hiyo ili kukamilisha dili lake la kujiunga na Yanga kwa ajili ya msimu ujao.

Akizungumzia shauku yake Litombo amesema: “Nasubiri kuanza kufanya kazi ndani ya Yanga, kama ambavyo unafahamu kila kitu tumemalizana na Yanga na kilichobaki kwa sasa ni kutambulishwa tu na kuanza kazi rasmi kuitumikia klabu yangu hii mpya.

“Kila kitu kuhusu mipango na malengo ya timu nayafahamu, hivyo na mimi nipo pamoja katika kuhakikisha tunayatizimiza malengo hayo kwa pamoja kwa kushirikiana.”


 

PAMOJA NA KUFANYA VIBAYA AKIWA NA YANGA..FARID MUSA ATAJWA NA STAR WA MOROCCO BIASHARA WAANZA KUJIWINDA KIMATAIFA…WAPANIA KUFIKIA MAFANIKIO YA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply