kimataifa

LEWANDOWSKI:INATOSHA KWA SASA KUWA NDANI BAYERN MUNICH

admin August 24, 2021 8:43 am


 MSHAMBULIAJI tegemeo ndani ya kikosi cha Bayern Munich, Robert Lewandowski amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba anahitaji kuondoka ili akapate changamoto mpya katika timu nyingine.

Nyota huyo yupo kwenye kiwango cha juu muda wote awapo ndani ya uwanja na asilima 90 ndani ya Bayern Munich amekuwa akiibuka kuwa mfungaji bora wa ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

Raia huyo wa Poland alianza kuweka wazi kwamba anahitaji kuondoka msimu uliopita lakini sasa ameanza kusema kwamba anahitaji kuondoka ili akapate changamoto mpya mahali pengine.

Ni Manchester City, Liverpool pamoja na Real Madrid zinatajwa kuwa na uhitaji wa kuipata saini yake hivyo akisepa ndani ya timu hiyo kuna uwezekano wa nyota huyo kuweza kuibukia kati ya timu hizo mbili.

“Nafikiri nataka chalenji mpya, nimefanikiwa kutwaa kila kitu nikiwa na Bayern na nafikiri sasa inatosha,” .

VIDEO: NEY WA MITEGO AZUNGUMZIA USAJILI WA YANGA BAADA YA KAMBI YA YANGA KUYEYUKA, NGUVU IMEELEKEZWA HUKU,SABABU ZATAJWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply