Yanga SC

KWA MWENDO HUU WA RIVER UNITED YA NIGERIA ..YANGA MJINDANE KISAIKOLOJIA LIGI YA MABINGWA

admin August 30, 2021 11:00 am


WAKATI Yanga ikipoteza mechi yake ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Zanaco jana kwa kufungwa bao 2-1, wapinzani wao kwenye kwenye michuano ya kimataifa, Rivers United ya Nigeria jana imeshinda 1-0 dhidi ya Akwa United.

Yanga na Rivers zitakutana Septemba 12 kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mechi ya Yanga bao la Yanga lilifungwa na mchezaji mshambuliaji wake mpya Heritier Makambo kwenye kipindi cha kwanza kabla ya kipindi cha pili Zanaco kusawazisha na kuongeza kupitia kwa Ackim Mumba na Kelvin Kapumbu.

Bao la wapinzani wa Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa lilifungwa na  Fortune Omoniwari dakika ya tisa ya mchezo huo baada ya kupokea pasi kutoka kwa winga Ishaq Kayode.

Na dakika ya 66 kipa wa Rivers, Theophilus Afelokai alionesha umahili wake wa kudaka kwa kuokoa mkwaju wa penati wa Akwa United na kuifanya timu yake ishinde 1-0 kwenye mechi hiyo iliyopigwa katika Dimba la Adokiye Amiesimaka.

VIDEO: MWINYI ZAHERA AIPA TANO YANGA, AMCHAMBUA BANGALA BAADA YA KUMALIZA MSIBA..BENO KAKOLANYA AWALILIA MASHABIKI WA SIMBA..AFUNGUKA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply