News

ACHANA NA BILIONI 2 ZA KUMUUZA LUIS….SIMBA SC WAANDIKA REKODI HII MPYA KWA AL AHLY

admin September 1, 2021 10:00 am


ACHANA na rekodi za kuwafunga kila mara wanapokanyaga kwenye Uwanja wa Mkapa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba imeandika rekodi nyingine dhidi ya Al Ahly ya Misri. Luis Jose waliyemuuza kwa Ahly kwa zaidi ya Sh2 bilioni amekuwa raia wa kwanza wa Msumbiji kucheza kwenye klabu hiyo kwa mujibu wa historia.

Hakuna mchezaji yeyote raia wa nchi hiyo aliyewahi kuchezea klabu hiyo kabla kwa mujibu wa rekodi zilizoko kwenye makumbusho ya Ahly jijini Cairo.

Lakini kwenye Ligi ya Misri anakuwa ni wa pili baada ya mkongwe wa ENPPI, Mano ambaye naye si mchezo.

Simba ilimuuza Luis baada ya Kocha Pitso Mosimane kushinikiza kwamba anamtaka baada ya kuona makali yake kwenye Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Habari za uhakika zinadai kwamba Wekundu hao walishindwa kuvumilia kuacha fedha za Ahly kwani ni nyingi ambazo wanaweza kufanyia mambo mengine ikiwamo kuvuta mashine mpya.

MOLINGA NI MALI YA NAMUNGO MUDA WA KUFANYA KWELI STARS NI SASA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply