News

RASMI…KIBU NA KISUBI NI MALI HALALI YA SIMBA SC…WAANZA KUKIPIGA NA WENZAO..

admin September 3, 2021 3:52 pm


WACHEZAJI wapya wa Simba, Jeremiah Kisubi na Kibu Denis rasmi wameanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzao leo asubuhi katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Wachezaji hao walikosekana katika kambi ya maandalizi kwaajili ya  msimu mpya iliyokuwa imewekwa nchini Morocco.

Gazeti la Mwanaspoti limeripoti kuwa limewashuhudia wachezaji hao wakiwa wananolewa na kocha mkuu Didier Gomes na na kocha wa viungo Adel Zrane.

Kibu alikuwa anacheza pamoja na wachezaji wengine kwenye programu za Gomes huku akiwa haonyeshi ugeni wowote ule.

Upande wa Kisubi alikuwa anafanya mazoezi ya pamoja  na Beno Kakolanya na Ally Salim.

Wachezaji waliokuwa kwenye mazoezi ni Jonas Mkude, Beno Kakolanya, Ally Salim, Hassan Dilunga, Cris Mugalu, Jimson Mwanuke, Lary Bwalya  na Gadiel Michael.

Wengine ni Kibu Denis, Ibrahim Ajibu, Pascal Wawa, Hassan Dilunga, Henock Inonga, Kennedy Juma, Benard Morrison, Sadio Kanoute, Joash Onyango, Abdulsamad Kassim, Pape Sakho na Duncan Nyoni.

SIMBA QUEENS YASHINDA 10-0 KIMATAIFA BAADA YA MANARA KUENDELEA KUICHARURA SIMBA…SIMBA SC WAIBUKA NA KUTOA TAMKO HILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply