Simba SC

SIMBA QUEENS YASHINDA 10-0 KIMATAIFA

admin September 3, 2021 2:43 pm


WAWAKILISHI wa Tanzania kwa upande wa Wanawake, Simba Queens leo wameibuka na ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya FAD FC.

Katika mchezo wa leo ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake, Simba Queens walitakata mapema kwa kuweza kutawala na kutumia nafasi ambazo walitengeneza.

Mpaka muda wa mapumziko ni mabao 7 kwa Simba na kipindi cha pili walifunga mabao matatu na kukamilisha idadi ya mabao 10 kwenye mchezo huo.

Watupiaji wa mabao ya leo ilikuwa ni Mawete Musolo aliyetupia mabao matatu,Opah Clement mabao matatu, Aisha Juma mabao mawili,Asha Djafar mabao mawili.

POLISI TANZANIA KUWEKA KAMBI MWANZA RASMI…KIBU NA KISUBI NI MALI HALALI YA SIMBA SC…WAANZA KUKIPIGA NA WENZAO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply