Michezo Bongo

Ukurasa Mpya Kwa Julio, Afichua Siri Ya Kuondoka Mashujaa

Vardo July 16, 2026 12:23 pm

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Jamhuri Kihweli (Julio), ameweka wazi sababu za kuondoka ndani ya klabu hiyo, akisema uamuzi huo umetokana na kutofautiana kwa baadhi ya matakwa kati yake na uongozi wa timu.

Kihweli amesema baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya awali, pande zote zilikutana tena kwa ajili ya kujadili mustakabali wake, ambapo aliwasilisha mahitaji yake.

Hata hivyo, mazungumzo hayo hayakuzaa mwafaka kutokana na kushindwa kufikia makubaliano kuhusu baadhi ya masuala muhimu.

“Kuna vitu ambavyo hatukukubaliana na ndiyo maana tumeachana na Mashujaa FC. Kulikuwa na mambo ambayo mimi niliyahitaji, lakini wao hawakuweza kuyatimiza, hivyo tumeamua kuachana kwa amani baada ya makubaliano ya pande zote mbili,” amesema Kihweli.

Kocha huyo amesisitiza kuwa hana kinyongo na klabu hiyo, akieleza kuwa anaondoka akiwa na heshima kubwa baada ya kushirikiana na uongozi na wachezaji katika kipindi ambacho timu ilikuwa inapitia changamoto.

Amesema anaamini mchango wake uliisaidia Mashujaa FC kuvuka kipindi kigumu na sasa yuko tayari kutafuta changamoto mpya katika safari yake ya ukocha.

Baada Ya kuwindwa Na Simba, Yona  Achagua Singida Black Stars Skudu Astaafu Kucheza Soka, Kituo Kinachofuata Ukocha