Yanga SC

Kamwe avunja ukimya, afichua siri ya Mabilioni yaliyomwagwa Yanga

Vardo July 16, 2026 11:55 am

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa umewekeza fedha nyingi katika dirisha hili la usajili kwa lengo la kujenga kikosi imara kitakachotetea mafanikio ya msimu uliopita na kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Msemaji wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe, amesema uongozi umelazimika kutumia fedha nyingi kuwasajili wachezaji wapya, huku baadhi yao wakinunuliwa baada ya kuvunja mikataba yao na klabu walizokuwa wakizitumikia.

Mbali na usajili huo, Kamwe amesema Yanga imeamua kuwabakiza baadhi ya nyota wake muhimu kwa kuwapa mikataba mipya yenye maslahi mazuri ili kuzuia wasiondoke na kuhakikisha msingi wa kikosi unaendelea kubaki imara kuelekea msimu wa 2026/27.

Amefafanua kuwa usajili uliofanywa umeongeza ushindani ndani ya kikosi, huku benchi la ufundi likipata chaguo pana katika maeneo mbalimbali ya uwanja. Pia amesema klabu imechukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa wamebakiza muda mfupi katika mikataba yao.

“GSM ameweka fedha nyingi za usajili maana wengi tumevunja mikataba na kununua wachezaji.Kuna wachezaji ambao tunawabakiza kwa kuwapa fedha nyingi, na pia tumewanunua wachezaji wapya kwa kuvunja mikataba yao.

Kuna wachezaji ambao mikataba yao imebakia muda mfupi, hivyo tumefanya usajili wa kutosha na kuongeza idadi ya wachezaji ndani ya timu,” amesema Kamwe.

Kauli hiyo inaonyesha dhamira ya Yanga ya kuendelea kuwa na kikosi chenye ushindani mkubwa, huku uongozi ukiamini uwekezaji uliofanywa katika usajili utaiwezesha timu kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho la CRDB pamoja na kufanya vizuri katika michuano ya CAF msimu wa 2026/27.

Meridian Scatter Whale Ni Ufalme Wa Bahari Unaofungua Milango Ya Burudani Na Ushindi Simba Wamtema, Singida Wamkumbatia Sowah